Ileje FM

Mwandishi wa habari akamatwa kwa kujifanya usalama wa taifa

May 6, 2024, 6:28 am

Kmanda wa jeshi la polisi mkoa wa Songwe Augustino Senga akizungumza na waandishi wa habari hawapo kwenye picha ( picha na Denis Sinkonde)

Na Denis Sinkonde,Songwe

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Songwe, Augustino Senga amesema wanamshikilia mwandishi wa habari (41) ambaye jina lake limehifadhiwa kwa kosa la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, akijitambulisha kuwa ofisa usalama wa Taifa.

Kamanda Senga ameyasema hayo Mei 05, 2024 alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

Kwa mujibu wa maelezo ya Kamanda Senga, mtuhumiwa huyo alikamatwa wilayani Momba mkoani humo kwa kujipatia fedha (kiusalama hajazitaja) akidai atawasaidia kushinda uchaguzi wa Serikali za mtaa kwa wananchi wenye nia ya kugombea.

sauti ya kamanda wa polisi mkoa wa Songwe Augustino Senga

“Alikuwa anatumia njia ya kuwakusanya baadhi ya wananchi akiwadanganya yeye ni ofisa usalama wa taifa na atawasaidia kushinda uchaguzi wa Serikali za mitaa, tumemkamata baada ya wasamaria wema kutoa taarifa kwenye vyombo vya usalama,”amesema kamanda Senga.

Kamanda Senga amesema kwa mtuhumiwa huyo alishafanya utapeli katika mikoa ya Dodoma, Njombe, Mbeya na Iringa kabla hajakamatwa Songwe ambapo pia alishafanya utapeli katika wilaya za Ileje na Momba.