Ileje FM

Wasichana 10114 wenye umri chini ya miaka 14 kupatiwa chanjo ya HPV

April 23, 2024, 4:25 pm

katika habari picha mkuu wa wilaya ya Ileje aliyevaa miwani wakati wa uzinduzi kampeni ya chanjo saratani ya mlango wa kizazi(picha na Denis Sinkonde)

Wasichana 10114 wenye umri chini ya miaka 14 wilayani Ileje Mkoani Songwe wanatarajia kupatiwa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi(HPV).

Katika uzinduzi huo ambao umefanyika leo April 23,2024 katika shule ya sekondari Ileje na Mkuu wa wilaya hiyo Farida Mgomi ambapo wazazi na walezi wameaswa kuwahamasisha kupata chanjo hiyo na kuepukana na imani potofu juu ya chajo hiyo kwani ipo salama.

Akizungumza katika uzinduzi wa chanjo hiyo Mkuu wa wilaya hiyo Farida Mgomi amewahakikishia mabinti hao kuwa kampeni ya chajo hiyo imethibitishwa shirika la afya dunuani(Who) na wizara ya afya kuwa ni salama hivyo mjitokeze kwa wingi kuchanja.

“Kutokana kwamba kampeni hii inawalenga waasichana waliopo sluleni na mtaani ni kuhakikisha viongozi ngazi ya vitongoji na vijiji pamoja na walimu mashuleni wanapewa elimu ya kutosha ili wasichana lengwa wanapatiwa elimu,” amesema Mgomi.

sauti ya mkuu wa wilaya ya Ileje Farida Mgomi

Amesema ugonjwa wa salatani ya mlango wa kizazi ni hatari hivyo wazazi hakikisheni watoto wenye umri wa miaka 9 mpaka 14 wanakuwa na kadi zile ambazo zinaonyesha wameshapatiwa chanjo ili kutambua ambao watakuwa hawajapata chanjo.

Mgomi amesema wazazi,viongozi ngazi ya wilaya, kata mpaka Kijiji na wataalamu wa afya wahakikishe wanaibeba ajenda ya chanjo hiyo ili kufikia lengo la wilaya kwa asilimia 100.

Mganga mkuu wa wilaya Ileje Joyce Ongati amesema zoezi la chanjo hiyo litafanyika kwa siku tano kuanzia Aprili 22 Jana tumefikiwa kuchanja wasichana 4571 sawa na asilimia 45.1 wakiwepo wasichana wa mtaani 24.

“Zoezi hili linaendeshwa katika shule za msingi na sekondari kulingana na umri uliolengwa pamoja na mtaani hivyo lengo la chanjo hiyo litafanikiwa kama ilivyopangwa,” amesema Ongati.

sauti ya mganga mkuu wilaya ya Ileje Joyce Ongati

Kwa upande wake afisa chanjo wa wilaya hiyo Raid Ngotezi amesema zoezi hilo litafanyika kwenye vituo 44 vya kutolea huduma za afya likisumamiwa na watoa huduma ngazi ya jamii, shule 115 zikiwepo shule za msingi 90 na sekondari 25.