Ileje FM

DC Ileje apiga marufuku kutumia vyandarua kujengea bustani

April 26, 2024, 4:27 pm

Mkuu wa Wilaya ya Ileje akigawa vyandarua hapo wakati wa maadhimisho ya siku ya malaria duniani (Picha na Denis Sinkonde)

Denis sinkonde, Songwe

Mkuu wa Wilaya ya Ileje mkoani Songwe Farida Mgomi amewaagiza viongozi wa serikali za vijiji wilayani humo kusimamia agizo la wananchi kutotumia vyandarua kwenye bustani za mbogamboga.

Mgomi ametoa agizo hilo wakati wa maadhimisho ya siku ya malaria duniani ambayo kwa wilaya ya Ileje yamefanyika katika zahanati ya Isongole kata ya Isongole kijiji cha Isongole na kuongeza zoezi la ugawaji vyandarua 480 kwa wamama wajawazito,watoto chini ya umri wa miaka 5 na watu wananoishi na virusi vya ukimwi.

Mgomi amesema wakati serikali inaendelea na jitihada za kupambana na Malaria nchini Kwa kugawa vyandarua vyenye dawa baadhi ya wananchi hugeuza matumizi yake na kukwamisha jitihada hizo.

Sauti ya mkuu wa wilaya ya Ileje Farida Mgomi

Aidha Mgomi ameipongeza Wizara ya Afya kwa kuanzisha mpango wa matumizi ya vyandarua vyenye viambata vya dawa ili kutokomeza mbu wanaosababisha vimelea vya malaria. 

Awali akisoma taarifa ya maadhimisho hayo Mganga Mkuu wa halmashauri ya Ileje Joyce Ongati amesema  

Sauti mganga mkuu wilaya ya Ileje Joyce Ongati