Ileje FM

Watu sita wakamatwa kwa kutoa mikopo ya kausha damu bila kibali

May 6, 2024, 6:52 am

kamanda wa polisi mkoa wa Songwe Augustino Senga akizungmza na waandishi wa habari hawapo pichani(Picha na Denis Sinkonde)

Na Denis Sinkonde,Songwe

Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe kwa kushirikiana na Benki Kuu ya Tanzania, wamewakamata watu 6, kwa tuhuma za kufanya biashara ya huduma za mikopo, maarufu kama ‘Kausha Damu’ bila kuwa na leseni, ambapo pia watu hao wamedaiwa kutoa mikopo kwa masharti magumu, ikiwemo kuchukua kadi za benki kama sehemu ya dhamana.

.Hayo yameelezwa na Kamnda wa Polisi Mkoa wa Songwe,  Augustino Senga, wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amebainisha kuwa katika kipindi cha mwezi Aprili 2024, Jeshi hilo limewakamata watuhumiwa 424 kwa tuhuma za makosa mbalimbali.

Katika kipindi hicho jeshi la polisi limewakamata watuhumiwa hao ambao walikuwa wanafanya kazi ya ukopeshaji fedha bila kuwa na kibali.

Sauti ya kamanda wa polisi mkoa wa Songwe Augustino Senga

Kamanda Senga ametoa rai kwa wananchi kufika jeshi la polisi kutoa taarifa pindi watakapowabaini watu wanaofanya ukopeshaji bila kuwa na kibali.