Ileje FM

Dc Ileje awapiga marufuku vijana kufanya mapenzi na wazee wao

October 11, 2023, 4:24 pm

Mkuu wa wilaya ya Ileje Farida Mgomi akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mtima (Picha na Denis Sinkonde)

Na Denis Sinkonde, Songwe

Mkuu wa wilaya ya Ileje mkoa wa Songwe Farida Mgomi amewapiga marufuku wanawake watu wazima kujihusisha na mapenzi na vijana wa kiume wenye umri mdogo.

Mgomi amesema hayo wakati wa mkutano wa kijiji Oktoba 10 mwaka huu katika kijiji cha Mtima wilayani hapa wakati wa kusikiliza kero za wananchi.

Mgomi amesema vitendo hivyo ni ukiukwaji wa maadili ya Tanzania na kuharibu vijana ambao ni nguvu kazi kwa taifa huku akilitaka jeshi la polisi na idara ya maendeleo ya jamii kutoa elimu.

sauti ya mkuu wa wilaya ya Ileje Farida Mgomi

Nao baadhi ya wananchi kijijini hapo wameelezea hisia zao juu ya tabia za wanawake hao.

Sauti za wananchi kijiji cha Mtima

Kijiji cha Mtima ni moja ya kijiji kinachounda kata ya Mbebe wilaya ya Ileje na kinapakana na nchi ya Malawi ambapo moja ya shughuli ya kiuchumi kwa wananchi  hao ni Kilimo.