Ileje FM
Ileje FM
19 May 2026, 11:34 am

Kutokana na tuhuma hizo za mwenyekiti wa kijiji imepelekea wananchi kuishi maisha ya hofu wakiogopa kufanyiwa vitendo viouvu katika shughuli zao za utafutaji
Na Denis Sinkonde,
Wanakijiji wa kijiji cha Shitunguru, kata ya Nambinzo, Wilaya ya Mbozi wameonesha kutoridhishwa na uwepo wa Mwenyekiti wa kijiji hicho kutokana na tuhuma mbalimbali zinazomkabili, zikiwemo kuwapa wananchi vitisho na kushindwa kutimiza majukumu yake ipasavyo.
Wakizungumza katika mkutano wa kusikiliza kero za wananchi uliofanyika chini ya uongozi wa Mkuu wa Wilaya ya Mbozi Hamad Mbega, wananchi hao wamelalamikia utendaji usioridhisha wa mwenyekiti huyo na kuomba aondolewe kwenye nafasi yake ya uongozi.
sauti ya wananchi wa kijiji cha Shitunguru
“Sisi hatumtaki mwenyekiti huyu ambaye anahatarisha maisha yetu kwa kututishia kutuchinja kwani anatembea na visu ,na ikionekana unamlalamikia kwa viongozi anaweka maisha yako hatarini” wamesema wananchi.

Akijibu hoja hizo, Mkuu wa Wilaya ya Mbozi Hamad Mbega ameagiza kufanyika kwa uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili mwenyekiti huyo, huku akisisitiza kuwa hatua za kusimamishwa kazi mara moja zitachukuliwa endapo itabainika kuwa tuhuma hizo ni za kweli.
Aidha, amewataka wananchi kufuata taratibu za kisheria katika kuendeleza mchakato wa kumuondoa mwenyekiti huyo kama walivyoomba awali.
sauti ya mkuu wa wilaya ya Mbozi