Ileje FM
Ileje FM
June 6, 2025, 7:31 am

Mamlaka ya udhibiti wa mbolea nyanda za juu kusini TFRA yatoa tahadhari kwa wafanyabiashara wanaovusha mbolea za ruzuku kwenda nchi za nje bial vibali.
Na:Denis Sinkonde
Wafanyabiashara na wamakala wa uuzaji wa pembejeo za kilimo ikiwemo mbolea ya ruzuku na mbegu katika Halmashauri ya Mji wa Tunduma na Ileje mkoani Songwe wametahadharishwa kujiepusha na uvushaji wa mbolea ya ruzuku kupeleka nchi jirani za Zambia na Malawi bila kufuata sheria kwani mamlaka hazitawafumbia macho.
Wito huo umetolewa na Meneja wa Mamlaka ya Udhibit wa Mbolea nyanda za juu kusini Joshua Ng’ondya katika mkutano uliowakutanisha mawakala pamoja na wafanyabiashara wa pembejeo hizo mkutano uliolenga kujadili changamoto zao ikiwa ni kuelekea msimu mpya wa kilimo.
Ng’ondya amewataka mawakala hao kujiepusha na uvushaji wa mbolea kupeleka nchi jirani bola kuwa na vibali , kwani kutorosha mbolea yenye ruzuku ni kukiuka kanuni na sharia za nchi hicyo ukikamatwa utashughulikiwa.
Amesema kama wafanyabiashara wamebaini fursa ya biashara ya mbolea nchi jirani ya Malawi wahakikishe wanaomba vibali kwani mamlaka ya udhibiti wa mbolea TFRA itawapa vibali ili kusafirisha mbolea hizo kwa mujibu wa sharia.
“Uti wa sheria bila shuruti utawafanya wafanyabiashara kufanya biashara kwa uhuru, licha ya kwamba Tunduma kuna changamoto kupungua niwasihi tufuate sharia zilowekwa hata kama mtakuta kunafursa upande wa pili ili kuepuka mkono wa sharia,” amesema Ng’ondya .
Ng’ondya amewataka wafanyabiashara wa mpakani maeneo ya Tunduma na Ileje kuhakikisha vibali vinazingatiwa kuliko kutumia njia ya panya iliyotolewa ruzuku na serikali tukiwabaini tutawachukulia hatua kali za kisheria.
“pia mbegu zote zipo kwenye mfumo wa rukuzu, najiuliza iwezje mfanyabiashara au wakala auze mbegu na mbolea nje ya mfumo wa utaratibu wa ruzuku ,niwasihi muache tabia hiyo mara moja kuuza mbolea ambazo ziko nje ya utaratibu na ndio maana kuna baadhi yenu kesi zipo kwenye vyombo vya sharia,”amesema Ng’ondya.
Aidha Ng’ondya amezitaka kampuni zinazojihusisha na biashara ya mbolea kuangallia namna ya kuongeza vifungashio vya kilo 10 hadi 5 ambayo imekuwa kero kubwa kwa wakulima sambamba na kutoa elimu juu ya matumizi sahihi ya mbolea husika ili kuondoa malalamiko kwa wakulima .
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa umoja wa mawakala wa uuzaji wa Mbolea mkoa wa Songwe Bashiri Hasunga wanakabiliwa na changamoto ya usambazaji wa mbolea kwa wakulima vijijini na mijijini kutokana na mawakala kupewa faida ndogo inayoachwa na makampuni kwa mawakala.
sauti ya makamu mwenyekiti wa mawakala wa mbolea
Hasunga ameitaka TFRA ipange bei elekezi kwa makampuni ya kuwauzia mawakala huku wakisema kuwepo zuio la makampuni kuwauzia wakulima mbolea moja kwa moja ili kulinda wafanya biashara wadogo na mitaji yao kwani wote ni walipakodi.
