Ileje FM

RUWASA Ileje walia na uharibifu wa mazingira

September 12, 2023, 7:51 am

Baadhi ya wanakamati wa jumuiya ya watumia Maji katika kijiji cha Mswima wakimsikiliza mkuu wa wilaya( Picha na Denis Sinkonde).

Na Denis Sinkonde, Songwe

Wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini RUWASA wilayani Ileje mkoani Songwe walia na changamoto ya uharibifu wa vyanzo vya maji hali inayopelekea baadhi ya miradi kutotoa maji kama ilivyokusudiwa. 

Hayo yamebainishwa na mratibu wa vyombo vya watumia maji wilayani hapa David Gunza  wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo kamati ya ulinzi ya usalama wilaya juu ya usimamizi wa utoaji huduma ya maji vijijini huku akitolea mfano chanzo cha maji Malangali , Shinji na Itale.

Sauti ya mratibu wa vyombo vya watumia maji Ileje David Gunza

Kwa upande wake Afisa maendeleo ya jamii wa mamlaka hiyo wilayani hapa Sifa Edom ameelezea changamoto ya ulipaji Ankara kwenye vituo vya maji.

Sauti ya afisa maendeleo ya jamii RUWASA Ileje Sifa Edom

Kutokana na changamoto hiyo mkuu wa wilaya ya Ileje ameuagiza uongozi wa RUWASA wilayani hapa kuorodhesha miradi iliyokamilika na isiyokamilika lengo ni kusaidiana kwa pamoja  kubaini kutatua changamoto zinazopelekea miradi hiyo kutowanufaisha wanainchi.

uongozi wa RUWASA wilayani hapa orodhesheni miradi iliyokamilika na isiyokamilika lengo ni kusaidiana kwa pamoja  kubaini kutatua changamoto zinazopelekea miradi hiyo kutowanufaisha wanainchi.

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Ileje Farida Mgomi