Ileje FM

Rc chongolo apongeza kasi ya mradi wa maji Ileje

April 30, 2024, 6:28 am

katika habari picha mkuu wa mkoa wa Songwe Daniel Chongolo aliyevaa kofia nyeusi akipokea maelekezo kutoka kwa meneja wa Ruwasa Ileje Mhandisi Endrew Tesha(Picha na Denis Sinkonde)

Na Denis Sinkonde,Songwe

Mkuu wa mkoa wa Songwe Daniel Chongolo ameipongeza Wakala Wa Maji na Usafi wa Mazingira (Ruwasa) wilayani Ileje mkoani humo kwa kasi ya utekelezaji wa mradi wa maji wa shilingi bilioni 4.9 utakaotatua changamoto ya maji Itumba ana Isongole.

Chongolo amesema  hayo April 29 mwaka huu wakati akikagua utekelezaji wa mradi huo katika chujio la mradi huo pamoja na tenki kubwa lenye ujazo wa lita laki tano(5,00,000).

Sauti ya mkuu wa mkoa wa Songwe Daniel Chongolo……

Kwa upande wake Menewa wa Ruwasa wilayani humo Mhandisi Endrew Tesha amesema mradi huo umefikia asilimia 85 hivyo wanahitaji fedha Sh 350 milioni kutoka ndani ya fedha za kutekeleza mradi huo.

“Kukamilika kwa mradi huo kutaondoa adha ya uhaba wa maji kwa wananchi 20,000 wa vijiji vya Itumba, Isongole, Ilulu na Izuba ambapo wamefanikiwa kuje ga tenki lenye ujazo wa lita laki tano pamoja na chujio la kuchuja maji,” amesema Mhandisi Tesha.

Sauti ya meneja wa Ruwasa wilaya ya Ileje Mhandisi Endrew Tesha……………….

Mkuu wa mkoa wa Songwe na Mkuu wa wilaya ya Ileje Farida Mgomi wakipanda ngazi kuelekea juu ya chujio maji la mradi wa maji Itumba Isongole(picha na Denis Sinkonde)