Ileje FM

DC Ileje aagiza machifu wapewe ushirikiano

October 3, 2023, 6:01 am

Mkuu wa wilaya ya Ileje Farida Mgomi akipokea zawadi kutoka kwa chifu wa tarafa ya Bulambya Simime Mwampashi(picha na Denis Sinkonde).

Na Denis Sinkonde

Mkuu wa wilaya ya Ileje mkoani Songwe Mhe.Farida Mgomi amewaagiza viongozi wa serikali wilayani humo kutoa ushirikiano na machifu kukemea matukio ya uvunjifu wa amani na uharibifu wa mazingira.

Mgomi amesema hayo Oktoba 2,2023 ikiwa ni siku ya kudumisha utamaduni ndani ya Wilaya, maadhimisho ambayo yameandaliwa na Umoja wa Jamii Tanzania (MUJATA).

Mgomi amesema viongozi wa serikali ngazi ya Kijiji,kata na tarafa kuacha tabia ya kudharau jitihada za machifu.

Sauti ya mkuu wa wilaya Ileje Farida Mgomi

Mgomi amesisitiza kuwa kila kiongozi atafanya kazi kwa mipaka yake, Viongozi wa Serikali watafanya kazi kwa mipaka yao na Viongozi wa Kimila nao watafanya kazi kwa mipaka yao.

Sauti ya mkuu wa wilaya Ileje Farida Mgomi