Ileje FM

Wananchi waliovamia maeneo watakiwa kuondoka

September 11, 2023, 12:51 pm

Wananchi waliovamia maeneo yaliyotengwa na wananchi katika kijiji cha Shinji wilayani Ileje mkoani Songwe watakiwa kuondoka

WANANCHI WA KIJIJI CHA SHINJI WAKIMSIKILIZA MKUU WA WILAYA ( picha na Denis Sinkonde).

Na Denis Sinkonde, Songwe

Agizo hilo limetolewa na mkuu wa wilaya hiyo Farida Mgomi wakati akizungumza na wananchi hao katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo huku kero kubwa ya wananchi ikiwa ni kuvamiwa maeneo waliyotenga.

Mgomi amesema uvamizi wa maeneo hayo ni kukiuka makubaliano ya wananchi hivyo watakaokutwa kwenye maeneo hayo hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.

sauti ya mkuu wa wilaya ya Ileje Farida Mgomi

Kwa upande wao wananchi wa kijiji hicho wameelekeza shutuma kwa mwenyekiti wa kijiji hicho kuruhusu uvamizi wa maeneo hayo.

sauti ya wananchi kijiji cha Shinji

Diwani wa kata hiyo John Mtafya ameiomba serikali ifanye utaratibu wa kuwasaidia wananchi.

sauti ya Diwani kata ya Mbebe John Mtafya