Ileje FM
Ileje FM
September 9, 2025, 6:08 am

Na Denis Sinkonde
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Augustino Senga amekabidhi jumla ya magari 6 mapya kwa ajili ya kuimarisha utendaji kazi wa Jeshi hilo hususani kuzuia na kupambana na uhalifu.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo fupi ya makabidhiano Septemba 8 mwaka huu, Kamanda Senga amewataka madereva wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe kuyatunza magari hayo kwa uangalifu mkubwa ili yaweze kutumika kwa muda mrefu.
sauti kamanda wa polisi mkoa wa Songwe Augustino Senga
Magari yaliyokabidhiwa ni pamoja na Toyota Land Cruiser Hardtop 5D, mawili ambayo yametolewa kwa matumizi ya Mkuu wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Songwe pamoja na Mkuu wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) Mkoa wa Songwe, huku Magari 3 aina ya Toyota Hilux Double Cabin yametolewa kwa ajili ya wakuu wa upelelezi wa makosa ya jinai katika Wilaya ya Mbozi, Momba na Songwe ikiwa ni pamoja na gari moja aina ya Land Cruiser GXR 300 Series kwa matumizi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe.
