Ileje FM

RC Songwe atangaza kiama wanaowapa mimba wanafunzi

April 29, 2024, 7:25 am

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Daniel Chongolo akizungumza na wanafunzi wa shule ya wasichana Ileje jana (Picha na Denis Sinkonde)

Na Denis Sinkonde, Songwe

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Daniel Chongolo amekemea vikali tabia ya uwepo wa mimba za utotoni hususani wanafunzi katika wilaya ya Ileje ambapo amesema katika utawala wake hakuna mtu yeyote atakayekwepa mkono wa dola kwa kumpatia mimba mwanafunzi.

Chongolo ameyasema hayo April 28 mwaka huu wakati akiongea na wananchi katika ziara yake eneo la Shule ya Sekondari ya Wasichana (Ileje Girls) iliyopo kijiji cha Ikumbilo kata ya Chitete wilayani Ileje.

“Niwaambie wala hatutaki kusema mengi ambao wao hawawezi kuacha mabinti wadogo wasome, tutawasaidia kwenda kufanya kazi zingine zitakazofaa zaidi ili wasionane na mabinti kwa miaka 10, 20, 25 mpaka 30 ili wakirudi wawe walimu wazuri.” amesema Chongolo

Mhe. Chongolo anatarajiwa kuendelea na ziara yake kesho kukagua miradi mbalimbali ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa ziara yake ya kikazi ya siku 4 ndani ya wilaya hiyo.