Ileje FM

Mliovamia hifadhi hekta 600 za hifadhi ondokeni haraka Dc Ileje

October 4, 2023, 7:15 am

Mkuu wa wilaya ya Ileje Farida akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ndapwa( picha na Denis sinkonde)

Na, Denis Sinkonde, Ileje

Wananchi vijiji vya Ndapwa kata Ngulilo wilaya ya Ileje mkoa wa Songwe na Kijiji Cha Kiobo wilaya ya Rungwe mkoa wa Mbeya wametakiwa kuondoka na kuacha na uvamizi kwenye hifadhi ya  msitu Kihosa uliopo Kijiji Cha Ndapwa wilayani Ileje Kwa kufuata kanuni na Sheria za misitu.

Agizo hilo limetolewa Oktoba 3,2023 na mkuu wa wilaya ya Ileje Farida Mgomi wakati akizungumza na wananchi wa Kijiji Cha Ndapwa kwenye mkutano wa hadhara kwenye kampeni ya oparesheni ya uhifadhi wa misitu uliondaliwa na ofisi ya wakala wa huduma za misitu Tanzania shamba la miti  Iyondo Mswima wilayani humo (TFS).

sauti ya mkuu wa wilaya Ileje Farida Mgomi

Kaimu Mhifadhi Mkuu wa Shamba la Miti Iyondo Mswima lililopo Wilaya ya Ileje Jovan M Emanuel amewahakikishia wananchi wa Kijiji cha Ndapwa  kuwa TFS itaanza zoezi la kugawa miche ya miti kwa wakazi wa eneo hilo mapema mwezi wa 12 ikiwa ni adhima ya kutekeleza dira ya uhifadhi wa mazingira lakini pia kuongeza kipato kwa wananchi.

sauti ya mhifadhi mkuu shamba la miti Iyondo Mswima Jovin Emanuel

Kaimu Mhifadhi Mkuu wa Shamba la Miti Iyondo Mswima Wilaya ya Ileje Jovan M Emanuel akitoa elimu kwa wananchi kijiji cha Ndapwa(picha na Denis Sinkonde)

Mwenyekiti wa kamati iliyochaguliwa Elius Cheyo amesema

sauti ya mwenyekiti kamati ya utunzaji uhifadhi wa mazingira Ndapwa Elius Cheyo

Meneja wa misitu wilaya ya Ileje Omary Abeid Ally akitoa elimu kwa wananchi wa Ndapwa(picha na (Denis Sinkonde)