Ileje FM

Wananchi Ileje waaswa kuudumisha muungano

April 26, 2024, 4:38 pm

Mkuu wa wilaya ya Ileje Farida Mgomi akizungumza wakati wa maadhimisho ya miaka 60 ya uhuru (picha na (Denis Sinkonde)

Na Denis Sinkonde,Songwe

Mkuu wa Wilaya ya Ileje mkoani Songwe Farida Mgomi, amewataka wananchi wa wilaya hiyo kuuenzi, kuulinda na kuutetea Muungano  kwa kushirikiana kufanya kazi kwa bidii juhudi na maarifa ili kuendelea kutunza na kuimarisha tunu za Muungano.

Mgomi, ameyasema hayo wakati wa maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliofanyika katika Ukumbi mpya halmashauri ya Ileje maarufu Community Center.

Mgomi amesema katika kipindi cha miaka 60 ya muungano wilaya ya Ileje imepokea fedha mbalimbali kutoka serikalini kwa kujenga na kuboresha miundombinu ya kutolea huduma ikiwepo elimu, afya ,maji, barabara pamoja na kuimarisha usalama.

sauti ya mkuu wa wilaya ya Ileje Farida Mgomi………………….

viongozi wa serikali,dini, wananchi na wanafunzi wakiwa katika ukumbi wa Communitu center wakati wa maadhimisho ya miaka 60 ya uhuru