Ileje FM
Ileje FM
1 October 2026, 2:22 pm

“Ni muhimu wananchi mkaepuka imani potofu juu ya lishe kwa mama na mtoto pamoja na umuhimu wa chanjo kwa watoto”.
Na Denis Sinkonde,Songwe
Wananchi wa Wilaya ya Songwe wametakiwa kuzingatia lishe bora kwa mama na mtoto katika siku 1,000 za kwanza, kuanzia kipindi cha ujauzito hadi mtoto kutimiza miaka miwili, kwa kuwa kipindi hicho ni muhimu kwa ukuaji na maendeleo ya mtoto.
Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Abubakar Kunenge, wakati wa ziara yake katika Wilayani Songwe, ambapo ametembelea Zahanati mpya ya Miembeni iliyoanza kutoa huduma kwa Wananchi.
Kunenge amekutana na akina mama waliowapeleka watoto wao kupata chanjo na kuwapongeza kwa kuzingatia afya zao.
“Niwasihi wananchi kuachana na imani potofu kuhusu matumizi ya vyandarua vyenye dawa, akieleza kuwa ni salama na havina madhara, hivyo kuwataka Wananchi kuvitumia ipasavyo katika kujikinga na malaria,” amesema Kunenge.
Kunenge amesema usipompelekea mtoto kupata chanjo inafika wakati anapooza na kupata magonjwa mbalimbali ikiwepo Maralia.