Ileje FM

6 October 2026, 6:23 am

Miradi 39 ya bilioni 14.48 kupitiwa na kukaguliwa na mwenge Songwe

Mkuu wa mkoa wa Songwe Abubakari Musa Kunenge akisoma taarifa ya miradi ya itakayopitiwa, kaguliwa na Mwenge wa uhuru kitaifa Mkoani Songwe(picha na Denis Sinkonde)

Mwenge wa uhuru umeanza mbio zake mkoani Songwe ukitokea Mkoani Mbeya

Na Denis Sinkonde,Songwe

Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Abubakar Mussa Kunenge, Oktoba 5, 2026, amepokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Jumanne Sagini, katika hafla ya makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru kati ya Mikoa ya Mbeya na Songwe makabidiano hayo yamefanyika katika halmashauri ya Songwe Kata ya Ifwekenya katika uwanja wa shule ya sekondari ifwekenya.

Mwenge wa Uhuru umepokelewa Mkoani Songwe na utakimbizwa kwa kipindi cha siku tano, kuanzia Oktoba 5,2026 hadi Oktoba 9,2026, ambapo utapita katika Halmashauri zote tano za Mkoa wa Songwe.

Mwenge wa Uhuru Ukiwa Mkoa wa Songwe utakimbizwa umbali wa kilomita 663.1 na utatembelea miradi 39 yenye thamani ya jumla ya Shilingi bilioni 14.48.

“Kati ya miradi hiyo, miradi 12 yenye thamani ya Shilingi bilioni 6.09 itawekewa mawe ya msingi, miradi 17 yenye thamani ya Shilingi bilioni 6.43 itazinduliwa, huku miradi 10 yenye thamani ya Shilingi bilioni 2.33 itakaguliwa,” amesema Kunenge.

sauti ya mkuu wa mkoa wa Songwe Abubakari Kunenge

Mwenge wa Uhuru mwaka 2026 umebeba ujumbe mkuu unaosema “AMANI, UMOJA NA MSHIKAMANO WA KITAIFA”, chini ya kaulimbiu isemayo: “Tanzania ni Yetu Sote, Tushikamane kwa Pamoja Kuleta Maendeleo.”

Mwenge wa Uhuru utaendelea kuwa sehemu muhimu ya kuhamasisha wananchi kuhusu amani, umoja, mshikamano wa kitaifa, utekelezaji wa miradi ya maendeleo na ushiriki wa wananchi katika kuleta maendeleo ya jamii.