Huheso FM

Huduma za afya zahanati ya Busangi zaboreshwa

February 26, 2025, 12:03 pm

Picha ya bomba la maji kwenye Zahanati ya Busangi ambayo miundombinu ya maji haikuwepo sasa imewekwa na maji yanapatikana muda wote.

Mwaka jana, Huheso Fm iliripoti changamoto za huduma za afya zinazoikabili Zahanati ya Busangi. Tuligundua kuwa changamoto ya Miundombinu ya maji ilisababisha Kwenda na maji yao kituoni jambo ambalo linakera wananchi; changamoto ya uhaba wa dawa ilisababisha wananchi kushindwa Kwenda kupata matibabu na changamoto ya usafiri wa dharura (ambulance) ilisababisha jamii kutokuona kipaumbele cha matibabu kwenye kituo hicho, Kufuatia ripoti hiyo, serikali ya halimashauri Msalala iliandaa mpango wa utekelezaji wa kushughulikia changamoto hizi.

Na Paschal Malulu

Huduma za afya nchini Tanzania ni muhimu kwa afya ya taifa letu. Huduma za afya zinapodorora, sote tuko hatarini. Mwaka jana, niliripoti kuhusu changamoto za huduma za afya zinazoikabili zahanati ya Busangi. Kutokana na ripoti hiyo, serikali ya wilaya ya Msalala ilitengeneza mpango kazi wa kukabiliana na changamoto hizo. leo tutaangalia hatua zilizochukuliwa hadi sasa na jinsi hali ilivyobadilika.