Huheso FM

Clouds Ndondo Cup kuanza kutimua vumbi Kahama Oktoba Mosi

September 14, 2023, 7:36 pm

Mashindano ya Clouds Ndondo Cup yanatarajiwa kufanyika mjini Kahama kuanzia Oktoba Mosi mwaka huu 2023 na usajili wa timu kushiriki wa timu utafungwa rasmi tarehe 22 Septemba 2023 na upangwaji wa makundi utafanyika Septemba 25, 2023 na kila kundi litakuwa na timu zisizozidi nne.

Picha ya Pamoja ya viongozi wa chama cha mpira wa miguu mkoa wa Shinyanga, chama cha soka Wilaya ya Kahama na baadhi ya viongozi wa timu zinazoshiriki michuano hiyo

Na Zakayo Isack-Kahama

MASHINDANO ya Ndondo Cup ambayo yanashirikisha vilabu vya timu za mpira wa miguu mitaani yanatarajia kuanza Oktoba Mosi 2023 wilayani Kahama mkoani Shinyanga kwa kushirikisha timu 16 zitakazojitokeza kwa mujibu wa utaratibu uliowekwa.

Akiongea na waandishi wa habari leo mratibu wa mashindano hayo, Yahaya Mohamed maarufu Mkazuzu ambayo pia yanadhaminiwa na Clouds Media amesema lengo la kutaka timu hizo ni kunyanyua vipaji wakiamini vinaanzia huko na vimekosa kuonekana au kuendelezwa.

Mohamed amesema mpaka sasa kuna vilabu vimejisajili kushiriki mashindano hayo kwa Mkoa wa Shinyanga na mwisho wa kuomba kushiriki mashindano hayo ni tarehe 22, Septemba,2023 huku akitaka viongozi wa vilabu vya mpira wa miguu wajitokeze.

“Mashindano haya kwa Sasa yamefikisha miaka kumi tangu kuanza kwake na yapo wazi kwa kila klabu kushiriki na kanuni za mpira ziko pale pale na mshindi atazawadiwa Sh milioni 5 na mshindi wa pili Sh milioni 3 na hakuna mshindi wa tatu”amesema Mohamed.

Mohamed amesema mashindano hayo katika maeneo yaliyofanyika yamekuwa na mvuto wa hali ya juu ambapo mashabiki wa timu watakao fanya vizuri katika ushangiliaji nao watapata zawadi na mshindi mmoja mmoja katika klabu aliyecheza atapata laki mbili na wachezaji watapewa jezi.

Katibu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Mkoa wa Shinyanga (SHIREFA)Marco Kaijage amesema vilabu vijitokeze visikatishe tamaa waratibu ,wameamua kuyachezea wilaya ya Kahama sio kwamba vilabu vya Kahama pekee bali yanahitaji vilabu vyote vilivyopo ndani ya mkoa huu.

Mwenyekiti wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Wilaya ya Kahama (KDFA) Hussein Salum amesema vilabu vya mpira wa miguu vijitokeze ni fursa kujitangaza na vilabu tisa vilivyojitokeza vingine vilikuwa vikisita kujisajili kwa kuwa na hofu huenda hayatakuwepo lakini leo mratibu amejitokeza Kahama vitazidi hitaji ya vilabu 16.

Kocha mkuu Frank Itohoro kutoka Mnarani Fc yenye Makazi yake kata ya Mhongolo amesema ni fursa kubwa kuja kwa Ndondo Cup kwani vijana wataonyesha vipaji vyao nakujitangaza wanaweza.

Kocha mkuu Shabani Ngogo kutoka Mbulu Fc yenye Makazi yake kata ya Nyasubi amesema mashindano hayo wameyasikia muda mrefu lakini mwaka huu yameletwa wilaya ya Kahama wameyapokea na maandalizi wameanza kuyafanya.