Huheso FM

Vijana washauri kujiajiri na kuacha kusubiri ajira za serikali

August 23, 2023, 2:00 pm

Kata ya kagongwa ni miongoni mwa maeneo ambayo yanasifika kwa mchanganyiko wa watu mbalimbali kibiashara.

Na Njile Ntelu

Vijana wa mtaa wa Iponya Kata ya Kagongwa Manispaa ya kahama mkoani Shinyanga, wamesema kuwa wameondokana na utegemezi wa ajira kutoka serikalini bali wameunda vikundi vya kusaidiana kupata mitaji ya kufanya shughuli za kibiashara.

Kata ya kagongwa ni miongoni mwa maeneo ambayo yanasifika kwa mchanganyiko wa watu mbalimbali kibiashara.

Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Iponya, Jointy William amesema vijana wa eneo hilo wamekuwa wakijishughulisha katika  kazi binafsi bila kutegemea serikali na kufanya kazi ambazo ni halali  katika jamii.

Sauti ya mwenyekiti serikali ya Mtaa wa Iponya Kata ya Kagongwa Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga

Kwa upande wao vijana wa eneo hilo wamesema kuwa wameamua kufanya kazi binafsi bila kutegemea serikali kwani kwa sasa ajira kutoka serikalini zimekua chache kulingana na watu wanaohitaji kuwa wengi hivyo baadhi yao wameanzisha kazi zao binafsi.

Sauti ya vijana waliojiajiri na kuunda vikundi vya kusaidiana katika Mtaa wa Iponya Kata ya Kagongwa

Hata hivyo mwenyekiti Jointy William amewaomba vijana kuchangamkia fursa zinazojitokeza katika maeneo wanayoishi ili kuwezesha kukidhi mahitaji ya kila siku bila kutegemea serikali.