Huheso FM

Madiwani Kahama wapongeza kukamilika miradi ya maendeleo

July 21, 2023, 1:00 pm

Madiwani wilayani Kahama mkoani Shinyanga wa meipongeza serikali ya awamu ya sita na halmashauri ya wilayani hiyo kwa juhudi za maendelo zinazofanyika katika mwaka wa fedha 2022/2023.

Madiwani wakiwa katika kikao cha baraza cha robo ya nne ya mwaka wa fedha 2022/2023: Picha Misoji Masumbuko

Na Misoji Masumbuko, Anas Ibrahim

Wameyasema hayo katika kikao cha madiwani cha robo ya nne ya mwaka wa fedha 2022/2023 kiliho fanyika kwenye ukumbi wa manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga

Madiwani hao wamesema baadhi ya miradi mingi ya maendeleo ikiwemo shule,barabara na masoko imeshakamilika na kunufaisha wakazi wa maeneo husika.ambapo awali walikuwa wakipitia changamoto

Sauti za Madiwani wakizungumza Katika kikao cha Baraza

Kwaupande wake Mbunge wajimbo la Kahama mjini Jumanne Kishimba ameipongeza serikali kwa kutoa fedha za miradi ya maendeleo ya wananchi.

Sauti ya Mbunge Jimbo la Kahama Jumanne Kishimba akizungumza kwenye baraza la Madiwani

Pamoja na hayo kikao hicho cha madiwani hao kimedhuhuriwa na viongozi mbalimbali wa halmashauri ya manispaa ya kahama.