Huheso FM

Wananchi walalamikia miundombinu ya barabara Kahama

March 6, 2024, 3:56 pm

Barabara inayolalamikiwa na wananchi kutuamisha maji Mtaa wa Mhongolo

Na, Neema NkumbiHuheso FM

Wananchi wa Kata ya Mhongolo Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga walalamikia miundombinu ya barabara kuwa mibovu wakati walipokuwa wakizungumzia kuhusu hali ya miundombinu ya Barabara.

Mmoja wa wananchi hao aliejitambulisha kwa jina Obed Nyangi amesema kuwa barabara nyingi za kuingia mtaani zina mashimo ambayo yanasababisha maji kutuama barabarani kwa muda mrefu ambapo inasababisha mazalia ya Mbu hali ambayo inapelekea maambukizi ya ugonjwa wa Malaria.

Pia Daniel Julias ambaye ni mwendesha pikipiki maarufu bodaboda amesema kuwa barabara za mitaani zimekuwa kero licha ya kwamba kuna magari makubwa ambayo yanabeba mizigo mikubwa yanapita hapo na kusababisha barabara kuwa mbaya.

Sauti ya wananchi wakilalamikia miundombinu ya Barabara

Hata hivyo mwenyekiti wa Mtaa wa Mhongolo, Emanuel Charles amesema kuwa kero hiyo imewasilishwa sehemu husika hivyo wananchi wawe wavumilivu wakati ambapo mamlaka husika zikishughulikia changamoto hiyo ya miundombinu.

Sauti ya mwenyekiti wa Mtaa wa Mhongolo akielezea miradi ya miundombinu ya barabara inayotekelezwa mtaani kwake