Huheso FM

Wanafunzi 12,120 Manispaa ya Kahama kufanya mtihani wa taifa juma lijalo

September 10, 2023, 2:25 pm

Picha ya mfano ya wanafunzi wakiwa darasani

Katika mtihani huo wanafunzi wenye mahitaji maalum katika Manispaa ya Kahama ni kumi ambao wanajumuishwa na wenye uoni hafifu.

Watahiniwa 12,120 wanaotarajiwa kuhitimu elimu ya msingi katika halmashauri ya Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga wanatarajiwa kufanya mtihani wa kitaifa wiki ijayo.

Akizungumzia mtihani huo Afisa elimu msingi Manispaa ya Kahama, Amida Kaganda amesema watahiniwa wanaotarajia kufanya mtihani huo utaanza Septemba 13 na 14   mwaka huu ambapo wavulana ni 5,463 na wasichana 6,657.

Amesema katika idadi hiyo inajumuisha wanafunzi wenye mahitaji maalum ikiwa wapo wenye uoni hafifu ambao ni wavulana  sita na wasichana  wakiwa 10.

Sauti ya afisa elimu msingi Manispaa ya Kahama, Amida Kaganda

Aidha Afisa elimu Amida Kaganda amewaomba wazazi kuwaandaa watoto kisaikorojia na kuwapatia mahitaji muhimu ili watoto wawe tayari kufanya mtihani kwani baadhi ya wazazi wamekua chanzo cha watoto kutokufanya vizuri katika mitihani yao.