Huheso FM

Wajumbe MTAKUWWA wapanga mikakati kupinga ukatili wa kijinsia

July 3, 2023, 12:24 pm

Wajumbe wa kamati ya MTAKUWWA wilayani Kahama mkoani Shinyanga wamekutana katika kikao  cha mradi wa Mwanamke Amka ili kujadili mpango kazi ambao utatokomeza ukatili wa kijinsia huku wanaume wakitajwa kuwa ndio chanzo kikubwa kinachochochea ukatili.

Wajumbe wa kamati ya MTAKUWWA wakipatiwa elimu ya ukatili wa kijinsia na namna ya kuripoti kesi za matukio hayo ndani ya jamii.picha Misoji Masumbuko

Na Misoji Masumbuko

Akizungumza wakati wa kikako kilichofanyika Ghama Hotel mratibu wa mradi wa Mwanamke Amka Joyce Michael amesema wanaume wanatakiwa kuwa wawazi na wakweli katika kuibua vitendo vya ukatili ambavyo vinafanyika kwenye jamii.

Sauti ya mratibu wa mradi wa mwanamke amka

wanaume wanatakiwa kuwa wawazi na wakweli katika kuibua vitendo vya ukatili ambavyo vinafanyika kwenye jamii

Kwa upande wao wajumbe wa kamati ya MTAKUWWA kutoka kata tofautitofauti wamesema wataendelea kutoa elimu kwenye jamii na kuwafikishia ujumbe ili waondokane na vitendo vya ukatili wa wanawake na watoto.

Sauti za wajumbe wa kamati ya MTAKUWWA

Kikao hicho kimejumuisha wanaume ambao ni wajumbe wa kamati ya MTAKUWWA na madereva bodaboda pamoja na maafisa maendeleo na watendaji kutoka katika kata za Mondo, Zongomela, Kinaga, Ngogwa na Kilago zilizopo wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

Muwezeshaji wa ukatili wa kijinsia akitoa mafunzo kwa wajumbe kuhusu ukatili wa kijinsia.picha Misoji Masumbuko