Huheso FM

Kishimba akabidhi mawe na fedha ujenzi wa Mitaro jimboni kwake

March 25, 2024, 1:13 pm

Mifuko ya saruji iliyokabidhiwa kwa ajili ya ujenzi wa mitaro

 Neema Nkumbi-Huheso FM

Mbunge wa Jimbo la Kahama mjini Mheshimiwa Jumanne Kishimba amekabidhi mifuko 50 ya saruji pamoja fedha shilingi milioni moja kwa ajili ya ujenzi wa mitaro unaoendelea Kata ya Majengo katika Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga.

Mifuko hiyo imekabidhiwa katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye ofisi za chama cha mapinduzi [ CCM] zilizopo Mtaa wa Majengo.

Sauti ya mbunge Jumanne Kishimba akizungumza kwenye mkutano wa kukabidhi mifuko ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa mitaro

Aidha Diwani wa Kata ya Majengo, Bernad Mahongo amempomgeza Mbunge Jumanne Kishimba kwa kuunga mkono juhudi mbalimbali za kiuchumi, elimu na mazingira katika Kata hiyo ya Majengo.

Sauti ya diwani Kata ya Majengo akizungumza wakati wa kukabidhiwa mifuko ya saruji