Huheso FM

Afisa mipango miji Kahama asimamishwa kazi

March 4, 2024, 3:06 pm

Picha ya mkuu wa Mkoa wa Shinyanga

“Huyu afisa alikuwa mpenzi wake na huyu mama kwahiyo penzi lilivyokufa huyu mama alikuwa anashindwa kudai haki yake ya kiwanja”

Na Paschal Malulu-Huheso fm

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Christina Mndeme amewasimamisha watumishi wanne wa halmashauri ya Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga kwa kuwa chanzo cha migogoro ya ardhi kwa wananchi.

RC Mndeme amesema kuwa watumishi hao wanasimamishwa ili kupisha uchunguzi juu ya tuhuma zinazowakabili ambapo katika watumishi hao yumo mkuu wa idara ya mipango miji Clemence Mkusya.

Sauti ya mkuu wa Mkoa akitoa tamko la kusimamishwa kazi watumishi wa idara ya ardhi