Huheso FM

Waendesha baiskeli mapacha wafariki Shinyanga

May 9, 2024, 8:59 pm

Mapacha waliofariki kwa ajali ya kugongwa na gari wakiwa kwenye pikipiki

“Tumepokea taarifa za kifo cha vijana wetu kwa masikitiko makubwa, wamefariki dunia kwa kugongwa na gari wakiwa watatu kwenye pikipiki. Inasikitisha sana watu waliozaliwa siku moja, wakafa siku moja, …tulikuwa tunawaandaa kwenda kushiriki mashindano nje ya nchi”

Waendesha Baiskeli Mabingwa wa Kanda ya Ziwa, mapacha Kulwa Mahega na Dotto Mahega wamefariki dunia kwa ajali kwa kugongwa na gari aina ya Land Cruiser wakiwa kwenye pikipiki eneo la Ndala Manispaa ya Shinyanga leo Alhamisi Mei 9,2024.

Mwenyekiti wa Chama cha Wapanda Baiskeli Mkoa wa Shinyanga Kashi Salula amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.