Huheso FM

Jamii kuishi kwa mazoea chanzo cha magonjwa yasioambukizwa

July 4, 2023, 10:56 am

Wananchi wa Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga wamesema magonjwa yasiyoambukizwa yamekuwa ni changamoto kutokana na maisha ya mazoea katika jamii.

Dkt. Flora Mwinuka akizungumza na mwandishi wa habari. Picha Misoji Masumbuko

Na Misoji Masumbuko

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wamesema watu wengi wanaopata magonjwa yasiyoambukizwa hawatambui mapema kutokana na kutokuwa na tabia ya kupima afya mara kwa mara.

sauti ya wananchi wakizungumza

Kwa upande wake Mratibu wa magonjwa yasiyoambukiza Dkt. Flora Mwinuka amesema wananchi wanapaswa kufika vituo vya afya mara kwa mara kuchunguza afya zao.

sauti ya Dkt. Flora Mwinuka

Hata hivyo amesema maadhimisho ya wiki ya magonjwa yasiyoambukizwa yameanza tarehe 7 mwezi huu na yanatarajia kufikia tamati tarehe 14 Novemba mwaka huu.