Huheso FM

Bandari tatu zatengewa Bilioni 60

August 31, 2023, 2:24 pm

Wandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga wakitembelea Bandari jijini Mwanza ambapo wametakiwa kutumia kalamu zao kuandika habari za fursa mbalimbali za Bandari kwa jamii

Waandishi wa Habari mkoani shinyanga wametakiwa kuwa mstari wa mbele kwenye jamii katika kuizungumzia Bandari na matumizi yake ili wananchi waweze kufahamu matumizi yake na umhimu wake.

Hayo yamesemwa na Afisa Bandari ya Isaka-Kahama mkoani Shinyanga, Abeli Mshang’a wakati akizunguzma na waandishi wa Habari wa Mkoa huo na kubainisha kuwa Bandari hiyo kavu imekuwa ikirahisisha utendaji wa bandari na inahudumia Nchi tano kusafirisha mizigo ikiwemo Rwanda,Burundi,Uganda,Sudani kusini,Na DRC.

Sauti ya Afisa Bandari ya Isaka Kahama mkoani Shinyanga, Abel Mshang’a

Kwa upande wake Meneja wa Bandari Ziwa Victoria Frednand Nyath amesema katika maboresho ya Bandari tatu za Mwanza kaskazini, Kemondo na Bukoba serikali imetenga Bilioni 60 kwa ajili ya kukarabati na maboresho hayo yataongeza ufanisi wa utendaji kazi bandarini.

Sauti ya Meneja wa Bandari ziwa Victoria, Frednand Nyath akizungumzia ukarabati wa Bandari zote tatu

Aidha miongoni mwa maboresho yanayotarajiwa kufanywa ni Pamoja na gati ya meli ya mizigo ya Gurudumu  na majengo ya abiria na kudhibiti mmomonyoko wa udongo kwa kuweka sakafu eneo hilo.