Huheso FM

Wamiliki wa nyumba za dada poa Kahama kukamatwa na wateja wao

March 4, 2024, 4:25 pm

Picha ya mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Christina Mndeme

Msiwakamate wanawake tu kamata wote anaejiuza na anaemnunua wote kamata weka ndani

Na Paschal Malulu

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Christina Mndeme ameagiza kukamatwa kwa watu wanaofanya biashara haramu ya ngono wilayani Kahama baada ya kushamiri kwa biashara hiyo na kuhusishwa na uhalifu.

Agizo hilo amelitoa baada ya kupokea malalamiko ya wakazi wa mtaa wa Majengo Manispaa ya Kahama ambao wamelalamikia kushamiri kwa biashara haramu ya ngono inayofanyika mchana na usiku katika nyumba za kulala wageni.

Sauti ya mkuu wa Mkoa wa Shinyanga

Wauzaji hukaa nje wakiwa nusu utupu ili kuwahamasisha wateja wao na mkuu wa Mkoa ameagiza wote wakamatwe pamoja na wateja wao wanapokutwa maeneo hayo.