Huheso FM

Waziri Mavunde afungua kituo cha mafunzo ya madini Kahama

March 18, 2024, 4:06 pm

Mavunde amesisitiza kuwa katika eneo la Buzwagi sambamba na kituo hicho cha Barrick Academy wananchi wazawa na watanzania kwa ujumla lazima wanufaike nalo na serikali inaendelea kuwakaribisha wawekezaji nchini kuwekeza hali itakayosaidia kuwakuza wachimbaji wadogo kwa kupatiwa mafunzo mbalimbali.

Na Neema Nkumbi-Huheso FM

Waziri wa Madini Antony Mavunde (mb) amezindua kituo cha mafunzo cha Barrick Academy wilayani Kahama mkoani Shinyanga chenye malengo ya kuongeza ubunifu na ujuzi wa wataalam katika sekta ya madini nchini.

Kituo hicho ambacho kipo ulipokuwa mgodi wa madini Buzwagi ambao umefungwa kutokana na kumaliza ushalishaji wa uchimbaji madini ya dhahabu, Waziri mavunde akiwa mgeni rasmi amesema kituo hicho cha mafunzo kitakuwa chachu ya kuongeza wataalam wa madini nchini.

Mavunde amesema kuwa kuwepo kwa kituo hicho ni dhamira ya dhati ya kampuni ya ucimbaji madini aina ya dhahabu Barrick katika kuwaendeleza watu mbalimbali kupata ujuzi ili kuendana na Sayansi na teknorojia katika sekta ya madini nchini ambapo watu wanaotarajiwa kupatiwa mafunzo ni 1024 kwa mwaka 2024.

Sauti ya waziri wa madini Antony Mavunde akizungumza wakati wa ufunguzi wa kituo cha mafunzo ya madini wilayani Kahama mkoani Shinyanga

Nae mbunge wa jimbo la Kahama mjini Jumanne Kishimba ameiomba kampuni ya Barrick kuhakikisha katika kituo hicho cha mafunzo cha Barrick Academy kuwasaidia wachimbaji wadogo wilayani Kahama ili kuwapatia ujuzi utakaosaidia ubunifu zaidi kwenye shughuli zao.

Sauti ya mbunge wa jimbo la Kahama mjini Jumanne Kishimba akizungumza wakati wa ufunguzi wa kituo cha mafunzo ya madini Kahama.

Kwa upande wake afisa mkuu wa uendeshaji wa Barrick katika kanda ya Afrika na Mashariki na kati, Sebastian Bock amesema kuwa kituo hicho kitakuwa kinatoa mafunzo kwa watu wote licha ya kipaumbele cha watanzania pia watakuwepo watu ambao watakuwa wanapatiwa mafunzo kutoka nje ya Tanzania kwa miaka miwili na watakaopatiwa mafunzo hayo ni zaidi ya watu 2000.

Sauti ya afisa mkuu wa uendeshaji wa Barrick kanda ya Afrika na Mashariki na kati, Sebastian Bock