Huheso FM

Ukarabati wa soko la Malunga kukamilika baada ya wiki mbili

July 14, 2022, 6:03 pm

Zoezi la ukarabati miundombinu ya soko la Malunga Mansipaa ya Kahama mkoani Shinyanga kwa ajili ya gulio linaendelea na linatarajiwa kukamilka wiki mbili zijazo.

 

Akizungumza na Huheso Fm leo julai 14, 2022 Mwenyekiti wa masoko na magulio manispaa ya Kahama, Bariki Daud amesema uwepo wa gulio hilo unatoa fursa kwa vijana na wananchi kujipatia kipato.

 

Daud amesema licha ya zoezi hilo kuendelea amewaomba wafanyabiashara wa soko hilo kuwa wavumilivu kutokana na  changamoto ambazo wanakutana  nazo katika ufukiaji wa mashimo inayopelekea kuwepo kwa vumbi na zoezi hilo litakamilika kwa haraka.

 

Aidha gulio hilo linatarajiwa kukamilika ndipo utaratibu wa ufanyikaji wa shughuli za biashara na namna ya wafanyabiashara ambavyo watapewa maeneo kwa ajili ya kufanya biashara.

Hata hivyo Wafanyabiashara wa soko hilo pamoja na wananchi wamepongeza ujio wa gulio kwani kutapanua wigo wa  biashaara na kuongezeka kwa wateja katika eneo hilo.