Huheso FM

Binti wa miaka 16 ajifungua, atembezewa kipigo na mumewe

September 11, 2024, 5:20 pm

Na Veronica Kazimoto-Huheso FM

Familia ya binti mwenye umri wa miaka 16 (jina limehifadhiwa) mkazi wa Nyihogo Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga aliyejifungua kwa oparesheni imelazimika kumchukua baada ya kufanyiwa ukatili wa kupigwa na mume wake huku akiwa hajapona.

Hayo yamethibitishwa Septemba 11, 2024 na balozi namba 23 Nyihogo, Charles Kashindye ambaye amesema ukatili huo umeanza muda mrefu na baada ya kujifungua, mume wake hakuacha kumfanyia ukatili huo.

Mjumbe wa serikali ya mtaa wa Nyihogo aliyemwakilisha mwenyekiti wa Mtaa wa Nyihogo, Eunice Epapira ametoa barua kwa binti huyo ili aweze kwenda nyumbani kwao kwa ajili ya usimamizi mzuri kwani ukatili kama huo ni kosa kisheria.

Sauti ya viongozi wa serikali ya mtaa wa Nyihogo wakizungumzia tukio la kupigwa kwa binti mwenye oparesheni ya uzazi na mume wake

Rehema Chindie moja ya mashuhuda wa tukio hilo amesema ukatili kama huo sio kitu kizuri kwani si vyema kwa afya kiujumla.

Sauti ya binti akizungumzia mkasa wote wa kipigo