Huheso FM

Mpangaji atelekeza kichanga ndani, chakutwa kimefariki

July 26, 2024, 5:25 pm

Mfano wa picha ya ramani ya kata ya Nyihogo

“Niliamka asubuhi nikaenda kwenye shughuli zangu nilivyorudi nikakuta mlango upo wazi nilivyoingia ndani kuangalia sikuona mtu kuangalia kitandani nikamuona mtoto yupo uchi nikashtuka kumuangalia mtoto wala hatikisiki nikamuita kijana wangu alipofika kumuangalia mtoto wala hapumui ”.

Na Rose Dominick, Neema Yohana na Lilian Francis

Mwili wa mtoto mchanga anayekadiriwa kuwa na umri wa wiki tatu hadi mwezi mmoja umekutwa umetelekezwa ndani ya nyumba ya mpangaji anayedaiwa kuwa mama wa kichanga hicho katika mtaa wa Nyihogo kata ya Nyihogo Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Julai 26, 2024 baada ya mama mwenye nyumba ajulikanae kwa jina Modesta Pima kuamka asubuhi kwa ajili ya kumwandalia chai mzazi wa kichanga hicho na alipoingia ndani aliukuta mwili wa mtoto ukiwa mtupu.

Amesema alivyomgusa mtoto aligundua kuwa amefariki na mama wa mtoto akiwa hayupo na hajulikani alipo.

Sauti ya Mama mwenye nyumba akieleza tukio kwa undani zaidi

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa wa Nyihogo, Iddi Mitimingi amekiri tutokea kwa tukio hilo ameeleza kuwa changamoto kubwa ipo kwa wamiliki wa nyumba kwani  hawazingatii mikataba ya upangishaji bali wameweka pesa kipaumbele.

Sauti ya Mwenyekiti Iddi Mitimingi akielezea tukio.

Jeshi la polisi baada ya kupata taarifa lilifika eneo la tukio na kuuchukua mwili wa kichanga hicho.