Uyui FM Radio

Idara ya ujenzi Manispaa ya Tabora rushwa imekithiri-Meya

14 January 2025, 12:41 pm

Madiwani wakiwa kwenye kikao cha kujadili rasimu ya bajeti 2025-2026.Picha na Zaituni Juma

“Kwasababu mkurugenzi upo na vyombo vipo vianze kuwashughulikia hawa watu mara moja”

Na Zaituni Juma

Vyombo ya usalama vimeagizwa kuchunguza idara ya ujenzi katika halmashauri ya Manispaa ya Tabora kufuatia kukithiri kwa vitendo vya rushwa hali ambayo imetajwa kuisababishia halmashauri kukosa mapato yake ya ndani na wakati mwingine kutofikia malengo iliyojiwekea.

Meya wa Manispaa ya Tabora Ramadhani Kapela ametoa agizo hilo wakati akiwa kwenye kikao cha baraza la madiwani lilipoketi kujadili rasimu ya bajeti ya mwaka 2025-2026.

Meya Ramadhani Kapela akizungumza kwenye baraza la madiwani.Picha na Zaituni Juma
Sauti ya Meya