Epuka matumizi yasiyo ya lazima-Dkt Mkama
14 January 2025, 11:49 am
Nidhamu ya muda na fedha imesisitizwa kwa yeyote anayetaka kufanikiwa.
Jamii Mkoani Tabora imetakiwa kuona umuhimu wa kuwa na nidhamu ya matumizi ya fedha ili kutimiza malengo wanayojiwekea kwa mwaka mzima.
Ushauri huo umetolewa na Mhadhiri wa chuo kikuu kishiriki cha Mtakatifu Agustino SAUT tawi la Tabora na mtaalamu wa saikolojia Daktari Ildefonce Mkama ambaye amesisitiza kuepuka matumizi yasiyo ya lazima.
Baadhi ya vijana Yusta fales na Elia Kivubu wametaja sababu zinazokwamisha katika kutimiza malengo waliyonayo.
Katika hatua nyingine Daktari Mkama ameiasa jamii kufanya tathmini ya malengo waliyojiwekea kila baada ya muda mfupi angalau miezi mitatu ili kutafuta suluhisho kwa vinavokwamisha malengo yao.