Tiba ya Himophilia kuanza kutolewa Tabora
8 January 2025, 11:39 am
Awaomba wataalam wa afya na wananchi kutumia klinik hiyo kwa kuibua wagonjwa wapya kwaajili ya kupata msaada.
Na Butungo Andrew
Hospitali ya rufaa mkoani Tabora Kitete kwakushirikiana na hospitali ya taifa Muhimbili pamoja na chama cha Himophilia Tanzania, imezindua klinik ya himophilia ambayo itajumuaisha utoaji wa matibabu kwa watu wanao ishi na ugonjwa huo.
Akizindua klinik hiyo Stella Lwiza ambae ni raisi wa chama cha himophilia nchini, amesema kuwa hadi sasa mradi huo umefanikiwa kuwatambuwa wagonjwa zaidi ya mia nne na umefanikiwa kutoa mafunzomkwa wataalamu wapya
Pia Stella amewaomba wataalamu wa afya na wananchi kuitumia klinik hiyo kwa kuibua wagonjwa wapya kwaajili yakupata msaada kuhusu tatizo hilo
Himophilia ni ugonjwa wa damu kukosa uwezo wakuganda unaosababishwa na ukosefu wakiwango chakutosha wa chembe chembe za protini ya kugandisha damu hali inayopelekea damu kuvuja kwa muda mrefu pale mgonjwa anapo pata jeraha