Wanasheria Tabora waiomba mahakama kuharakisha kesi
8 January 2025, 11:12 am
Mwenyekiti wa chama cha mawakili kanda ya Tabora Kelvin kayaga akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kero ya wafungwa kukaa muda mrefu mahabusu
Wanasheria Tabora waazimia kutopokea majarada ya msaada wa sheria ndani ya miezi sita hadi kesi zisikilizwe kwa wakati.
Na Augustino Ntyangiri
Chama cha wanasheria Tanganyika Kanda ya Tabora wamelaani na kukemea vitendo visivyo vya haki vinavyo fanywa na mahakama ya kiuchunguzi kwa kuwashikilia watuhumiwa kwa muda mrefu bila kuwafikisha mahakamani.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa chama cha mawakili kanda ya Tabora Kelvin kayaga wakati akizungumza na vyombo vya habari january 7, 2025 mkoani humo
Aidha Kayaga ameongeza kuwa kutokana na hali hiyo wameazimia kutoshiriki na kupokea majarada ya msaada wa sheria ndani ya miezi sita hadi mamlaka zitakapo chukua hatua stahiki
Hayo yamejiri baada ya wakili wa kujitegemea hassani kilingo kufanyiwa tukio lisilo la kiungwana january 1, 2025 na jeshi la poisi ambapo alizuiliwa kutoonana na wateja wake