Uyui FM Radio

Watu wawili wakutwa wamefariki kwenye chumba kimoja

6 December 2024, 9:35 pm

Miili ikitolewa kwenye nyumba kwaajili ya kuepelekwa kuhifadhiwa hospital.picha na Mohamed Habibu

Jeshi la polisi linaendelea kufanya uchunguzi ili kubaini sababu ya kifo hicho

Na Salma Abdul

Watu wawili wakutwa wamefariki katika chumba kimoja mtaa wa Majengo kata ya Ipuli manispaa ya Tabora.

Kwa mujibu wa taarifa watu hao waliofariki ni PETER MASALI  na MWATANO huku wakidhaniwa kuwa na mahusiano ya kimapenzi.

Angle ni mmoja wapangaji wa marehemu PETER MASALI anazungumzia jinsi ilivyokuwa .

Sauti ya mpangaji

Nao baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo ambao ni majirani akiwemo Mzee Shabani na  Ester Makito wamesema wao walisikia taarifa kuwa kuna watu wawili wamekutwa wamefariki ndani ndipo kutoa taarifa kwa Uongozi wa mtaa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa mtaa wa Majengo, kata ya Ipuli manispaa ya Tabora Jumanne  Kazimoto  amelezea alivyopokea taarifa hizo.

Mwenyekiti wa mtaa wa majengo akizungumza na wanahabari.Picha na Mohamed Habibu
Sauti ya mwenyekiti

kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora SACP Richard Abwao amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Kamanda wa polisi mkoa wa Tabora SACP Abwao akizungumza na waandishi.Picha na Mohamed Habibu