Uyui FM Radio

Shekhe asimamishwa kwa kuratibu ndoa bandia

12 July 2024, 5:14 pm

Shekh wa Mkoa Mavumbi akiwa na viongozi wengine wa BAKWATA.Picha na Allan Ntana

Suala hilo limetokea kutokana na mpango wa mfadhili kuwatafuta vijana kwa lengo la kuwafungisha ndoa na kugharamia mahari pamoja na mambo mengine.

Na Zaituni Juma

Baraza  la Mashehe mkoani Tabora limemsimamisha kazi  Shekhe wa kata ya Mtendeni Manispaa ya Tabora Bakari Sikonge, kwa kukiuka maadili na kuratibu ndoa kwa mtu ambaye tayari alishafunga ndoa awali.

Akizungumzia suala hilo Shekhe wa Mkoa wa Tabora  Ibrahim Mavumbi amesema kuwa mbali na kusimamishwa pia wataendelea kufuatilia mienendo yake ili kujiridhisha kama amebadilika au la.

Shekh wa Mkoa wa Tabora Ibrahimu Mavumbi.Picha na Allan Ntana
Sauti ya Shekh wa mkoa

Amesisitiza kuwa baraza litaendelea kufuatilia mienendo ya viongozi hao na endapo itabainika kuwa wana mengine wanayofanya kinyume na maelekezo hatua za kinidhamu zitachuliwa dhidi yao.