Uyui FM Radio

Kampuni za tumbaku zatakiwa kuwalipa wakulima kwa wakati

1 July 2023, 6:32 pm

Serikali imetakiwa kuhakikisha kampuni zinazonunua tumbaku za wakulima wanalipwa kwa wakati.

Rai hiyo imetolewa na mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Tabora na mjumbe wa kamati kuu ya halmashauri kuu ya CCM Taifa Hassan Wakasuvi.

Baadhi ya wananchi wakiwa viwanja vya Fatma Mwasa -Maonesho ya ushirika

Akitolea ufafanuzi wa changamoto hiyo Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amesema hadi sasa shilingi bilioni 400 zimelipwa na makampuni ya ununuzi wa tumbaku.

Waziri Bashe akiwa kwenye maonesho ya wiki ya ushirika kitaifa- Tabora

sauti ya waziri Bashe

Kwa upande wake mstahiki meya wa manispaa ya Tabora Ramadhan Kapela amesema maadhimisho ya siku ya ushirika kufanyika mkoani Tabora kitaifa kumeinua uchumi.