Uyui FM Radio
Idara ya ujenzi Manispaa ya Tabora rushwa imekithiri-Meya
14 January 2025, 12:41 pm
“Kwasababu mkurugenzi upo na vyombo vipo vianze kuwashughulikia hawa watu mara moja”
Na Zaituni Juma
Vyombo ya usalama vimeagizwa kuchunguza idara ya ujenzi katika halmashauri ya Manispaa ya Tabora kufuatia kukithiri kwa vitendo vya rushwa hali ambayo imetajwa kuisababishia halmashauri kukosa mapato yake ya ndani na wakati mwingine kutofikia malengo iliyojiwekea.
Meya wa Manispaa ya Tabora Ramadhani Kapela ametoa agizo hilo wakati akiwa kwenye kikao cha baraza la madiwani lilipoketi kujadili rasimu ya bajeti ya mwaka 2025-2026.