Uyui FM Radio

Epuka matumizi yasiyo ya lazima-Dkt Mkama

14 January 2025, 11:49 am

Dkt Ildefonce Mkama akizungumza kwenye kipindi cha Kifungua kinywa.Picha na Zaituni Juma

Nidhamu ya muda na fedha imesisitizwa kwa yeyote anayetaka kufanikiwa.

Jamii Mkoani Tabora imetakiwa kuona umuhimu wa kuwa na nidhamu ya matumizi ya fedha ili kutimiza malengo wanayojiwekea kwa mwaka mzima.

Ushauri huo umetolewa na Mhadhiri wa chuo kikuu kishiriki cha Mtakatifu Agustino SAUT tawi la Tabora na mtaalamu wa saikolojia Daktari Ildefonce Mkama ambaye amesisitiza kuepuka matumizi yasiyo ya lazima.

Sauti ya Mwanasaikolojia

Baadhi ya vijana Yusta fales na Elia Kivubu wametaja sababu zinazokwamisha katika kutimiza malengo waliyonayo.

Sauti za vijana

Katika hatua nyingine Daktari Mkama ameiasa jamii kufanya tathmini ya malengo waliyojiwekea kila baada ya muda mfupi angalau miezi mitatu ili kutafuta suluhisho kwa vinavokwamisha malengo yao.