Watu wawili wakutwa wamefariki kwenye chumba kimoja
6 December 2024, 9:35 pm
Jeshi la polisi linaendelea kufanya uchunguzi ili kubaini sababu ya kifo hicho
Na Salma Abdul
Watu wawili wakutwa wamefariki katika chumba kimoja mtaa wa Majengo kata ya Ipuli manispaa ya Tabora.
Kwa mujibu wa taarifa watu hao waliofariki ni PETER MASALI na MWATANO huku wakidhaniwa kuwa na mahusiano ya kimapenzi.
Angle ni mmoja wapangaji wa marehemu PETER MASALI anazungumzia jinsi ilivyokuwa .
Nao baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo ambao ni majirani akiwemo Mzee Shabani na Ester Makito wamesema wao walisikia taarifa kuwa kuna watu wawili wamekutwa wamefariki ndani ndipo kutoa taarifa kwa Uongozi wa mtaa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa mtaa wa Majengo, kata ya Ipuli manispaa ya Tabora Jumanne Kazimoto amelezea alivyopokea taarifa hizo.
kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora SACP Richard Abwao amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.