Uyui FM Radio

Watumishi wa umma watakiwa kuzingatia uadilifu

23 October 2024, 4:48 pm

Baadhi ya wajumbe wakiwemo madiwani wakiwa kwenye kikao.Picha na Nyamizi Mdaki

Mfumo mpya wa manunuzi NEST umetajwa kuondoa urasimu na kuongeza uwajibikaji.

Na Nyamizi Mdaki

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Paul Chacha amezitaka taasisi zinazojihusisha na manunuzi mbalimbali kuzingatia maadili wakati wa kusimamia na kugawa zabuni zinazotangazwa.

Mkuu wa Mkoa ameeleza hayo alipowakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Uyui Mohamed Mtulyakwaku kwenye baraza maalumu la madiwani wa wilaya ya Uyui lililolenga kutoa elimu ya matumizi ya mfumo mpya wa manunuzi wa NEST.

Sauti ya mkuu wa wilaya ya Uyui

Naye, Meneja wa mamlaka ya udhibiti wa manunuzi kanda ya kati na Magharibi Mhandisi Suma Mwanjwango amesema amesema mfumo wa kielektroniki wa ununuzi wa umma utazuia mianya ya rushwa.

Sauti ya mhandisi Mwajwango

Nao, Diwani wa kata ya Goweko Shaban Katalambula,Diwani viti maalum Janeti Sita,pamoja na diwani wa kata ya Isikizya Ally Mtelela wanazungumzia kuhusu maadili.

Sauti za madiwani