Viongozi wa dini Tabora wahamasisha uandikishaji
18 October 2024, 2:52 pm
Zoezi la kujiorodesha katika daftari la mpiga kura kwaajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa linafikia tamati oktoba 20 mwaka huu.
Na Nyamizi Mdaki
Wananchi Mkoani Tabora wakumbushwa kwenda kujiandikisha ili wapate sifa za kuwachagua viongozi wanaowahitaji.
Rai hiyo imetolewa na kadhi wa mkoa wa Tabora Shehe Ibrahim Said akisema kwamba faida moja wapo ya kupiga kura ni kuondoa kinyongo nafsini.
Kwa upande wake mchungaji wa kanisa la Anglikana Tanzania Dayosisi ya Tabora David Bilusha ambae pia ni mratibu wa kamati ya amani na mahusiano ya dini mkoani hapa amewataka waumini kujitokeza bila kukatishwa tamaa na jambo lolote.
Nae katibu wa BAKWATA Mkoa wa Tabora Mohamed Abed ameendelea kutoa hamasa kwa wananchi kujiandikisha kwani ni haki yao kikatiba.