Uyui FM Radio

Dc Mtulyakwaku: Nendeni mkajiorodheshe mpate viongozi bora

17 October 2024, 5:01 pm

Wananchi waliofika kituoni kwaajili ya kujiorodesha.Picha na Nyamizi Mdaki

Na Nyamizi Mdaki

Mkuu wa Wilaya ya Uyui Mkoani Tabora Mohamed Mtulyakwaku amesema nyumba nzuri inaendana na msingi imara hivyo wananchi wanapaswa kujiorodesha kwenye daftari la orodha ya wapiga kura ili wapate viongozi bora.

Mtulyakwaku ametoa rai kwenye uzinduzi wa zoezi hilo lililofanyika katika kitongoji cha Taifa Road kata ya Isikizya.

Mkuu wa wilaya ya Uyui akijiandikisha.Picha na Nyamizi Mdaki

Naye, Afisa uchaguzi wilaya ya Uyui mwalimu Amosi Wigaye ametaja sifa za mtu anayepaswa kujiandikisha kwenye orodha hiyo.

Kwa upande wao wananchi wa wilaya hiyo,Hadija Juma,Julius Shija,Hadija Rashid na Omary Salanyanzaka wamesema

Zoezi la uandikishaji kwenye daftari la orodha ya wapiga kura limeanza Oktoba 11 hadi Oktoba 20 2024.