Shilingi milioni 10 zachangwa na wananchi kujenga daraja
24 September 2024, 4:32 pm
Katika eneo hilo wananchi wamekuwa wakipata tabu ya kuvuka hususasni kipindi cha masika na kusababisha maafa ya watoto,kuibiwa na vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Na Salma Abdul
Wananchi wa kata ya chemchem Manispaa ya Tabora wamechangia fedha na nguvu kazi kwenye ujenzi wa kivuko cha daraja katika eneo la mto kenge.
Wananchi Amani Bugama ,Fatuma Kasim na Muhidini Almas wamezungumzia adha walizokuwa wakipata pindi wanapovuka kwenye kivuko hicho cha daraja.
Naye mwenyekiti wa mtaa wa Baruti kata ya chemchem Jumanne Hamad amesema ujenzi wa daraja hilo ni ushirikiano wa wananchi kujitolea fedha na mahitaji mbalimbali ikiwemo mchanga, kokoto ,mawe na gharama ya fundi fedha hizo zimetolewa na wananchi.
Naye diwani wa kata ya chemchem Alhaj Kasongo Amran amewashukuru wananchi kwa kujitolea kukamilisha ujenzi wa daraja hilo ambalo ilikuwa ni moja ya changamoto kutokana na matukio ya uhalifu na baadhi ya watoto kufariki dunia kwa kusombwa na maji.
Ujenzi wa kivuko hicho cha daraja umegharimu zaidi ya shilingi milioni 10 fedha ambayo imetolewa na wananchi wa kata ya chemchem Manispaa ya Tabora kupitia mikutano ya hadhara na kuona ujenzi huo ni kipaumbele.