Uyui FM Radio

Wapeni nafasi vijana kuwaongoza-katibu wazazi CCM Tabora

29 August 2024, 6:12 pm

Baadhi ya wananchi wa mtaa wa subira wakiwa kwenye mkutano.Picha na Zaituni Juma

Baadhi ya jamii zimekuwa na mtazamo hasi kuwa vijana hawawezi kushika nafasi mbalimbali za uongozi

Na zaituni Juma.

Jamii imetakiwa kuona umuhimu wa vijana  kuongoza nafasi mbalimbali kwani wao pia wana uwezo wa kutatua matatizo yanayowakabili wanachi wa maeneo husika.

Wito huo umetolewa na  mwenyekiti wa mtaa wa subira kata ya Chemchem Manispaa ya Tabora Rashidi Amani ambae amesema ilikuwa vigumu kwake kuaminiwa na jamii kutokana na mitazamo hasi iliyopo kwa baadhi ya watu.

Mwenyekiti wa mtaa wa subira akiwa katika studio za Uyui fm radio.Picha na Zaituni Juma
Sauti ya Rashidi Amani

Akizungumzia suala hilo katibu wa jumuiya wazazi chama cha mapinduzi CCM  wilaya ya Tabora johari Amani ametoa wito kwa viongozi ambao wamehudumu nafasi  za uongozi ikiwemo ngazi za mitaa kwa muda mrefu kutoa fursa kwa vijana.

Katibu wa wazazi CCM Tabora mjini akizungumza na wananchi wa mtaa wa subira.Picha na Zaituni Juma
Sauti ya katibu wazazsi CCM Tabora mjini

Mwenyekiti wa mtaa wa Subira Rashidy Amani amewasisitiza vijana wanapoaminiwa na jamii katika kuwaongoza kuwa wabunifu na kuwatumikia kwa weledi ili kuleta maendeleo.