Hospitali wilaya ya Tabora yapata vifaa tiba
14 August 2024, 9:56 am
Vifaa tiba vilivyotolewa vina thamani ya zaidi ya shilingi milioni sita.
Na Salma Abdul
Mkuu wa mkoa wa Tabora Paul Chacha amepokea vifaa tiba ikiwemo viti mwenda pamoja na vitanda kwaajili ya kusaidia utoaji wa huduma mbalimbali za matibabu katika hospitali ya wilaya ya Tabora.
Akipokea msaada huo kutoka benki ya NMB tawi la Mihayo Tabora mkuu wa mkoa wa Tabora ameshukuru na kuahidi kuwa vitatunzwa vizuri.
Meneja wa benki ya NMB kanda ya magharibi Restus Assenga amesema wametoa vifaa hivyo baada ya kupokea maombi kutoka katika hospitali hiyo.
Agness Mathias ni mmoja wa wananchi walioshuhudia upokeaji wa vifaa hivyo ambaye ni miongoni mwa wanaopata huduma katika hospitali hiyo amesema.
Naye Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo Daktari Gwamaka Edward ametoa shukrani kwa kupatikana kwa vifaa hivyo.